WADAU WAITHIBITISHA MPANGO WA JUMLA WA USIMAMIZI WA USIMAMIZI WA MAENEO TENGEFU YA DAR ES SALAAM
Jumanne Juni 16, 2026 Dar es Salaam
_1781634950.jpeg)
Kaimu Meneja Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Bw. Davis Mpotwa amefungua warsha ya siku mbili inayofanyika kuanzia tarehe 16 Juni hadi 17 Juni,2026 katika ukumbi wa Manespaa ya Temeke Dar es Salaam, kwa lengo la kuthibitisha Mpango wa Jumla wa Usimamizi (General Management Plan- GMP) wa Maeneo Tengefu ya Dar es Salaam (DMRS). Katika Hotuba yake Bw. Mpotwa amempongeza mtaalam mshauri kwa kukamilisha rasimu ya GMP pamoja na wadau wote waliochangia katika maandalizi yake. Aidha amezishukuru Taasisi za WIOMSA na Nairobi Convection kwa ushirikiano uliowezesha kukamilika kwa kazi hio muhimu.
Hata hivyo Bw. Mpotwa amesisitiza kuwa uhifadhi wa maeneo unamchango mkubwa katika kuhifadhi bioanuawai, kulinda ukanda wa pwani, kusaidia shughuli za uvuvi, kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari. Aliendelea kwa kusema kuwa “ushikishwaji wa wadau umeongeza uthabiti wa GMP kwani maoni ya pamoja na ushirkiano ni nyenzo muhimu katka kufanikisha uhifadhi enedelevu wa bahari”.
Warsha hii imekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wenye viti wa kamati za Usimamizi wa Uvuvi wa Fukwe (BMU), wahifadhi wa kujitolea, wawakilishi wa Taasisi za Umma, wadau wa uhifadhi wa mazingira pamoja na watendaji wa kata.
Akizungumza katika maohiano mafupi Mtendaji wa Kata ya Mji Mwema- Kigamboni Bi. Jane Lugangira amewataka washiriki wa warsha hiyo kuwa mabalozi wa uhifadi kwa kuendelea kutoa elimu umuhimu wa kulinda mazingira ya bahari na kuhamaisisha matmizi endelevu ya rasilimali zake. “Ulizi wa bahari ni jukumu letu sote, tutafanikiwa kwa kuendelea kushirikiana bega kwa bega na kutoruhusu vitendo vinavyo haribu mazingira ya bahari”, alisema Bi Jane.
kwa upande wake Mwenyeki wa BMU Mtaa wa ferry Bw. Seif Ismail amesema ana imani kubwa na GMP ya Maeneo Tengefu ya Dar es Salaam kuwa utaleta matokeo chanya katika usimamizi wa maeneo ya uvuvi na maeneo ya mazalia ya samaki na kwa watumiaji wote wa rasilimali za bahari, amesema “tunaahidi kutoa ushikiano katika utekelezaji ili kufikia malengo kusudiwa ya mpango huu, uandajii wa mpango umekua shirikishi tangu awali hadi kufikia hatua hii ya ukamilishwaji”.

