WAFANYAKAZI MIMP WAPATIWA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA KIDIJITALI WA TAARIFA ZA MIAMBA YA MATUMBAWE

Alhamisi, June,05, 2025, Mafia
Wafanyakazi wa Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP) na Hifadhi ya Maeneo Hai (Biosphere Reserve) wamepatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa Kidijitali wa Kitaifa ujulikanao kama “Tanzania Coral Reef Database System”.
Mafunzo hayo yaliyotolewa Juni, 05, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa MIMPBR na kuongozwa na Afisa TEHAMA, Bw. Abasi Maige yanalenga kuboresha ukusanyaji, Uhifadhi na uchakataji wa taarifa muhimu kuhusu Miamba ya Matumbawe na Bioanuai kwa ujumla wake, samaki na wanajamii nchini Tanzania.
Aidha, Matumizi ya mfumo huu mpya wa kidijitali unatarajia kuboresha utunzaji muhimu wa kumbukumbu wa taarifa, ufanisi na kuchochea uwajibikaji kwa wafanyakazi katika kutekeleza shughuli za kulinda na kusimamia Rasilimali za Bahari katika Maeneo yaliyohifadhiwa ya Bahari (MPAs).