WATAALAM KUTOKA BENKI YA DUNIA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA MPRU
WATAALAM KUTOKA BENKI YA DUNIA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA MPRU

Jumanne, Machi 25 2025, Dar es Salaam

Wataalam kutoka Benki ya Dunia (World Bank) kupitia mradi wa TASFAM wametembelea Makao Makuu ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) ili kujifunza na kujulishwa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na MPRU ikiwemo utekelezaji wa sheria na kanuni za uhifadhi Bahari  kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Tanzania hivi karibuni itaanza kutekeleza Mradi wa TASFAM (Tanzania Scaling up Sustainable Marine Fisheries and Aquaculture Management) utakaofadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo katika ziara hiyo wataalamu walipata fursa ya uelewa kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji wa sheria wa  usimamizi wa rasilimali za bahari na kuthibiti uvuvi haramu. 

Lengo ni kuhakikisha na kuona kuwa Mradi wa TASFAM unaboresha sekta ya uvuvi kwa kuwa na uvuvi endelevu na kulinda rasilimali za bahari.

Ziara hii inaashiria hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, wahisani, na wadau wa Uhifadhi wa mazingira ya Bahari kwa lengo la kufanikisha malengo ya Uhifadhi na maendeleo endelevu.