WATANZANIA WAPATIWA FURSA YA KUJIFUNZA JUU YA UHIFADHI WA MATUMBAWE KUPITIA USOMAJI WA KIDIJITALI
WATANZANIA WAPATIWA FURSA YA KUJIFUNZA JUU YA UHIFADHI WA MATUMBAWE KUPITIA USOMAJI WA KIDIJITALI

Jumanne, Oktoba 08, 2025, Dar es Salaam

Watanzania wamepatiwa fursa ya kujifunza juu ya Uhifadhi wa Miamba ya Matumbawe kupitia usomaji wa kimtandao (kidijitali) katika Mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili Mustakabari wa Uhifadhi wa Matumbawe na Utekelezaji ambapo Tanzania ni moja ya nchi ambayo ina aina ya  Matumbawe  yanatopatikana katika Ukanda wa Magharaibi mwa Bahari lakini kwa ujumla katika nchi saba zinazitekeleza mradi huu wa Uokoaji wa Matumbawe.

Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania Bw. Davis Mpotwa akizungumza pembezoni mwa Mkutano huo uliofanyika Oktoba 08, 2025 katika Hoteli ya Peacock iliyopo jijini Dar es Salaam alisema Tanzania ni Moja ya nchi ambayo ina aina ya Matumbawe  yanayopatikana katika Ukanda wa Magharibi mwa Bahari lakini kwa ujumla katika nchi saba zinazotekeleza mradi huu wa Uokoaji Matumbawe. 

"Kikao cha leo kinalenga kutoa fursa kwa watanzania kujifunza juu ya uhifadhi wa matumbawe kupitia usomaji wa kimtandao unaweza kujisajili kupitia mtandao kwa kushare link kutoka taasisi mbalimbali za serikali na wataenda katika vyuo vyao na mashirika yao kuhakikisha  kwamba  kijana wakitanzania  anapata fursa ya kusoma kozi za online zinazohusu matumbawe na jinsi gani ya kuhifadhi matumbawe na kutumia taaluma za kisayansi kuhakikisha matumbawe yanalindwa  na kuhifadhiwa" Alisema Bw. Mpotwa.

Pia amesema kuhakikisha mazalia ya samaki yanaendelea kuwepo kwa kizazi cha sasa na kijacho na kuthamini kile ambacho wamefanya katika miaka hii mitatu iliyopita katika utekelezaji wa mradi kwa pamoja  huku wwakiendelea kutekeleza kwa mwaka wa nne katika kipindi hiki.

Hata hivyo amesema yapo mambo ambayo wamekubali kuyafanya ikiwa ni pamoja na kutengeneza mfumo portal, ambao utasaidia wanasayansi wote na wahusika wa masuala ya baharini hususan katika masuala ya matumbawe kuwa sehemu ambayo wanahifadhi taarifa zao pamoja na kupakua taarifa  kutoka  sehemu mbalimbali duniani na kuzitumia kwaajili yakuhakikisha kwamba jamii inazipata.

Sanjari na hayo pia amewaasa waandishi wa habari pamoja na jamii nyingine kuwa wana fursa ya kuingia  katika mfumo portal kupata taarifa mbalimbali hususan zinazohusu bahari, uchafuzi wa mazingira ili kuwa na takwimu halisi wanapotoa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama magazeti, tovuti au sehemu mbalimbali kama majukwaa kwa ajili ya jamii.

Naye Mtafiti na Mwalimu kutoka Chuo Kikuu Cha KilImo cha Sokoine Rose Kicheleri  amesema mradi umewasidia  kupata taarifa muhimu ambazo zitasidia  sana kufanya maamuzi ya uhifadhi wa matumbawe pamoja na kuendeleza matumbawe nchini .

Amesema  wamehusika katika  tafiti mbalimbali na kupata taarifa ambazo ni nzuri na zote zinasaidia  hasa tafiti za matishio na fursa  ambazo zinatokana na Matumbawe hasa uelewa wa wadau kutoka ngazi tofauti kuhusu matumbawe,  mfano matishio na fursa nyingi sana hizi zinaendana na uchimi wa Buluu  kwa Tanzania Bara  bado hazijaweza kuchukuliwa  na wadau mablimbali lakini kwa Zanzibar fursa hizi zinachukuliwa kwa nguvu.

"Matishio ni kazi za kibinadamu pamoja na mabadiliko ya tabianchi hizi zinakua katika kazi tofauti kutika ngazi ya chini kabisa kwa wananchi wanatumia matumbawe kupata samaki.

Kwa upande wake Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  Bi. Upendo Hamidu amesema kwamba  wanaangalia ushiriki wa makundi maalumu hasa wanawake na vijana kwenye kusimamia Matumbawe hasa athari  zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia shughuli za tabia nchi zinazo haribu.

Amesema mazalia ya samaki yanasababisha kutupatia kiapato pamoja na ulonzi wabahari lakini chamgamoto zinaathiri wadau mbalimbali waliopo kwenye jamii.