WATUMISHI MPRU, WADAU WASHIRIKIANA KUFANYA ZOEZI LA USAFI KATIKA KISIWA CHA MBUDYA
WATUMISHI MPRU, WADAU WASHIRIKIANA KUFANYA ZOEZI LA USAFI KATIKA KISIWA CHA MBUDYA

Alhamisi, 16 Mei 2024, Dar es Salaam

Watumishi kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameshiriki zoezi la usafi wa mazingira katika fukwe la Eneo Tengefu la Kisiwa cha Mbudya katika juhudi za kuhakikisha utunzaji safi wa mazingira pamoja na uhai wa rasilimali na viumbe vinavyopatikana Baharini.

Zoezi hilo la usafi katika Kisiwa cha Mbudya limefanyika ikiwa ni kutokana na athari zilizochangizwa na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha mfululizo ambapo zilisababisha kutenga taka nyingi sana pembezoni mwa fukwe na kuchafua mandhari safi ya mchanga wa fukwe katika eneo la Kisiwa hicho.

Kuelekea Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa tarehe 05/06/2024 duniani kote MPRU kama wahifadhi wa rasilimali za Bahari wanalo jukumu la kuhakikisha maeneo yake ya uhifadhi yanatunzwa katika njia ya usafi kama njia endelevu ya kuchochea sera ya uchumi wa buluu.

Wadau mbalimbali walioshiriki katika zoezi hilo la usafi wa mazingira katika fukwe ya Kisiwa cha Mbudya walikuwa ni Sana Mare, Mazingira Plus, Blue Green Heroes, African Reflections Foundation, Global Ecology Restoration Foundation, MBRC The Ocean, Sustainable Ocean Alliance (SOA Tanzania), Hudefo, Climate Care Organisation na Proffer Foundation.