WATUMISHI WATATU (3) MPRU-TMRS WAPATIWA MAFUNZO YA UREJESHAJI WA MIAMBA YA MATUMBAWE

Jumanne, September 16, 2025, Zanzibar
Watumishi watatu (3) kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) kituo cha Tanga Marine Reservation System (TMRS) wamefanikiwa kumaliza program ya mafunzo ya Urejeshaji wa Miamba ya Matumbawe (Coral Reef Restoration) yaliyofanyika kwa muda wa siku kumi kuanzia Septemba 1-10, 2025 katika fukwe iliyopo Jambiani, Zanzibar.
Mafunzo hayo yalishirikisha watumishi watatu (3) kutoka MPRU-TMRS akiwemo Bw. Jacob Edes, Bw. Emmanuel Madeni pamoja na Bw. Uchimbila ambapo waliweza kupatiwa ujuzi kuhusu Urejeshaji wa Miamba ya Matumbawe ikiwa ni hatua muhimu ya kuhakikisha ulinzi na ustawi wa viumbe hai wa baharini na usimamizi endelevu wa rasilimali zake.
Mafunzo hayo yalifadhiliwa na The East African Crude Oil Pipeline Project (EACOP) na kutekelezwa na Wildlife Conservation Society (WCS).