WATUMISHI WATATU (3) WA TACMP (TMRS) WAKAMILISHA MAFUNZO YA UZAMIAJI NGAZI ZA ‘OPEN WATER’ NA ‘ADVANCED OPEN WATER DIVING’ MKOANI TANGA
WATUMISHI WATATU (3) WA TACMP (TMRS) WAKAMILISHA MAFUNZO YA UZAMIAJI NGAZI ZA ‘OPEN WATER’ NA ‘ADVANCED OPEN WATER DIVING’ MKOANI TANGA

Jumatatu

Watumishi watatu (3) kutoka Hifadhi ya Bahari Tanga Silikanti (TACMP/TMRS) Bw. Jacob Kagasha Edes, Juma Hussein Uchimbila pamoja na Emmanuel Alphonse Madeni wamekamilisha mafunzo ya uzamiaji kwa ngazi za ‘Open Water’ na ‘Advanced Open Water’ ambapo mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa siku (9) kuanzia Julai 10-18, 2025 katika Mkoa wa Tanga.

Programu hiyo ya mafunzo ilifadhiliwa na East African Crude Oil Pipeline (EACOP) kwa kushirikiana na Wildlife Conservation Society (WCS) ambao walitekeleza programu hiyo ya mafunzo ya kina, ikijumuisha ujuzi muhimu kama vile uongozi wa majini, kudhibiti uzito chini ya maji, na mbinu za usalama, imemuwezesha kila mshiriki kupata zana za kushiriki kikamilifu katika juhudi za uchunguzi na urejeshaji wa Miamba ya Matumbawe.

Aidha, watumishi hao kupitia ujuzi walioupata katika mafunzo hayo utawaongezea umahiri katika kuendelea kulinda mifumo ya baharini (eco-system), ikiwemo Miamba ya Matumbawe,ambayo ni muhimu kwa uhai wa viumbe vya Baharini na pia kwa kupunguza athari za Mabadiliko ya Tabianchi.