WWF YAIKABIDHI MPRU MABOYA 24 NA GPS 2
WWF YAIKABIDHI MPRU MABOYA 24 NA GPS 2

Dkt. Modesta Medard (kulia) kutoka shirika la Uhifadhi Duniani (WWF) amekabidhi vifaa vyenye thamani zaidi ya Milioni Saba kwa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) ili kuendeleza ufanisi wa Taasisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Vifaa hivyo ni pamoja na Maboya (Life jackets) 24 na vifaa viwili maalumu vya kutambua maeneo kijiografia vijulikanavyo kama GPS. Vyote hivi vitatumika katika shughuli za doria, ufuatiliaji wa rasilimali za bahari (monitoring), uokoaji na kuweka alama na mipaka ya baharini na nchi kavu (boundary demarcation) pamoja na shughuli nyingine za kijamii.

Dkt. Modesta Medard ambaye ni Mratibu wa wa mipango ya Bahari - WWF ameeleza kuwa vifaa hivyo vimefadhiliwa kupitia mradi wa WWF-BAF 2019-2024 unaotekelezwa katika ukanda wa Rufiji, Mafia na Kilwa (RUMAKI Seascape).

Aidha kwa upande wake Bw. Mohamed Shamte kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania ameishukuru WWF Tanzania kwa kuunga mkono juhudi na jitihada za utunzaji wa rasiliamali za bahari kwa matumizi endelevu katika kukuza uchumi wa buluu, aidha Bw. Shamte ametoa rai kwa Mashirika na Taasisi nyingine kuiga mfano wa WWF katika uhifadhi wa bahari na matumizi endelevu ya rasilimali zake.