ZOEZI LA KUHUISHA MIPAKA YA KANDA ZA UHIFADHI KATIKA HIFADHI YA BAHARI MAFIA
ZOEZI LA KUHUISHA MIPAKA YA KANDA ZA UHIFADHI KATIKA HIFADHI YA BAHARI MAFIA

Jumanne, 29 Mei 2024, Mafia

Hifadhi ya Bahari ya Mafia kwa kushirikiana na vijiji vilivyopo ndani ya hifadhi imeanza kutekeleza zoezi la kuhuisha mipaka ya matumizi rasilimali za baharini ikiwa ni sehemu ya maboresho katika kuhifadhi maeneo ya bahari katika eneo la Mafia. Zoezi la uwekaji wa alama ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali unaotaka maeneo yote ya hifadhi kuwekewa alama na kusimamiwa ili kuepusha migogoro na kuwezesha usimamizi wa rasilimali za bahari.

Mradi wa Blue Action Fund (BAF) unaosimamiwa na World Wildlife Fund (WWF) umewezesha ununuzi wa alama za mboya ya kisasa yapatayo tisa (9) na minyororo 126.