KAIMU MENEJA MPRU ASHIRIKI WARSHA YA MPANGO KAZI WA KITAIFA WA KASA WA MAJINI (2024-2029)
KAIMU MENEJA MPRU ASHIRIKI WARSHA YA MPANGO KAZI WA KITAIFA WA KASA WA MAJINI (2024-2029)

Jumatatu, 13 Mei 2024, Dar es Salaam

Kaimu Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania (MPRU) Bw. Davis Mpotwa ameshiriki warsha ya wadau iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Seasense kwa ushirikiano na Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID) inayolenga kusambaza Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kasa wa Majini 2024-2029. 

Mpango huu unasisitiza wajibu wa pamoja wa kuhifadhi Kasa wa baharini  huku ikiwa ni asilimia 1 tu ya watoto wa Kasa wanaoanguliwa hadi kufikia umri wa kuzaa, hivyo inahitajika hatua za haraka ziweze kuchukuliwa ili kuweza kukabiliana na changamoto hii. 

MPRU ambao wanayo dhamana ya kusimamia rasilimali endelevu za shughuli za uhifadhi wa viumbe wa baharini wakiwemo Kasa kwa kushirikiana na wadau watahakikisha jitihada za dhati za kuzuia kutoweka kwa viumbe hawa wa ajabu na kuhakikisha uhai wao kwa ajili ya vizazi vijavyo.