MPRU YAONESHA MAFANIKIO YA UHIFADHI SHIRIKISHI KATIKA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA 2026
MPRU YAONESHA MAFANIKIO YA UHIFADHI SHIRIKISHI KATIKA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA 2026

Agosti 01, 2026                Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Agosti 1, 2026, amezindua Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Viwanja vya John Malecela- Nzuguni, Dodoma, ambapo Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) ni miongoni mwa washiriki katika eneo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

 

Kupitia ushirikiano na Shirika la GIZ, MPRU imewezesha ushiriki wa wanajamii wanufaika wa uhifadhi wa bahari kutoka Hifadhi za Bahari Tanga na Mafia kwa lengo la kuonesha matokeo ya shughuli mbadala za kiuchumi zinazochochewa na uhifadhi wa rasilimali za bahari.

Wanajamii hao wanawakilishwa na vikundi vinavyojishughulisha na uvunaji wa asali inayotokana na mikoko kutoka Wilaya ya Mkinga katika Maeneo Tengefu ya Tanga (TMRS), pamoja na Kikundi cha Kiupe kutoka Kijiji cha Kiegeani kilichopo ndani ya Hifadhi ya Bahari ya Mafia (MIMP) wanaojihusisha na uchakataji wa zao la mwani.

 

Ushiriki wao unatoa fursa ya kutangaza bidhaa zao,kutanua soko na kubadilishana uzoefu na kuonesha namna uhifadhi unavyochangia kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka hifadhi.

Sambamba na hilo, MPRU inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa rasilimali za bahari, fursa za shughuli mbadala za kujiongezea kipato katika maeneo ya hifadhi, uwekezaji unaozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za bahari pamoja na utalii wa ekolojia.

slot gacor