RC MTWARA ASISITIZA UHIFADHI MAENEO TENGEFU
RC MTWARA ASISITIZA UHIFADHI MAENEO TENGEFU

Jumamosi, Septemba 5, 2026        Msimbati

Mkuu wa Mkoa Wa Mtwara Mhe. Kanali Donald Msengi amefungua msimu wa nyangumi kwa mwaka 2026 kwenye tukio lililofanyika Septemba 05,2026 kwenye hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (MBREMP) iliyopo eneo la Msimbati mkoani humo.

 

Akizungumza katika tukio hilo Kanali Msengi amesema kuwa tukio hilo mbali na kuwavutia wengi kwa kushuhudia mnyama huyo mkubwa kuliko wote ulimwenguni linatumika kutoa elimu ya uhifadhi wa Maeneo Tengefu ili kuendeleza kulinda rasilimali za bahari.

“Tunafungua msimu wa Nyangumi 2026 ambao utaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Novemba ambapo hii inafungua ukurasa mpya wa wajibu wetu wa kulinda bahari, nyangumi na kutengeneza fursa endelevu za utalii kwa wananchi wetu hapa Mtwara na Tanzania kwa ujumla” Amesema Kanali Msengi.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Dkt. Bonaventure Baya amesema kuwa MBREMP ni miongoni mwa hifadhi tatu na maeneo Tengefu 15 yanayosimamiwa na MPRU, ambapo amebainisha kuwa uhifadhi wa bahari unajumuisha ulinzi wa mazingira, shughuli za uvuvi na utalii, fukwe za bahari, Ukuzaji viumbe maji na shughuli nyingine zinazotegemea rasilimaji ya maji.

 

Msimu huo wa nne wa Nyangumi utaendelea hadi mwezi Novemba mwaka huu wakati Nyangumi hao wakihama kutoka ghuba ya mnazi kuelekea katika eneo jingine la bahari ya hindi.

slot gacor