TEKNOLOJIA NA TAKWIMU KUIMARISHA USIMAMIZI WA HIFADHI ZA BAHARI
TEKNOLOJIA NA TAKWIMU KUIMARISHA USIMAMIZI WA HIFADHI ZA BAHARI

Ijumaa, Septemba 18, 2026    Mafia

 

Wataalamu wa uhifadhi kutoka Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) na Idara ya Uhifadhi wa Bahari (DMC) wamejengewa uwezo wa kutumia takwimu na teknolojia katika kuimarisha ufanyaji wa maamuzi kupitia warsha ya Adaptive Management iliyofanyika Septemba 14–18, 2026 katika Ukumbi wa Jerusalem, Kilindoni, Mafia.

 

Warsha hiyo iliyobeba dhana ya “From Theory to Practice” imelenga kuunganisha nadharia za usimamizi unaobadilika kulingana na taarifa zinazopatikana (adaptive management) na utekelezaji wake kwa vitendo katika maeneo ya hifadhi za bahari.

 

Katika mafunzo hayo, washiriki walifanya mazoezi ya vitendo ya uchoraji wa ramani na ufuatiliaji wa maeneo kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drones) pamoja na simu janja, huku wakijifunza namna ya kutumia taarifa zinazokusanywa katika kufanya maamuzi ya usimamizi na uhifadhi.

 

Aidha, MPRU na DMC zimepokea ndege mbili zisizo na rubani kutoka Swedish Agency for Marine and Water Management (SwAM), zitakazotumika katika kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa katika maeneo ya hifadhi za bahari Tanzania Bara na Zanzibar. Warsha hiyo imewakutanisha watumishi wa maeneo ya hifadhi za bahari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, hatua inayolenga kuimarisha matumizi ya teknolojia na takwimu katika usimamizi wa maeneo ya hifadhi za bahari.

slot gacor