MDAHALO WA NGAZI YA JUU WAANGAZIA MUSTAKABALI WA UHIFADHI NA UCHUMI WA BULUU
Jumamosi Septemba 26, 2026 Mafia

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) imeongoza Mdahalo wa Ngazi ya Juu katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 30 ya Hifadhi za Bahari nchini na Tamasha la Kisiwa cha Mafia, yaliyofanyika leo, Septemba 26, 2026, katika eneo la Utende, Mafia.
Mdahalo huo uliowakutanisha wawakilishi wa Serikali, Ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU), pamoja na wahifadhi wa bahari wastaafu na waliopo kazini, umejadili masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni kuimarisha uhifadhi shirikishi, matumizi ya teknolojia katika usimamizi wa rasilimali za bahari, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi na kukuza uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu.
Katika kilele cha maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Kamani, alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

