MPRU YAONGOZA MDAHALO WA MIAKA 30 YA UHIFADHI WA BAHARI MAFIA
MPRU YAONGOZA MDAHALO WA MIAKA 30 YA UHIFADHI WA BAHARI MAFIA

Ijumaa Septemba 25, 2026        Mafia

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) inaongoza mdahalo maalum kuelekea maadhimisho ya Miaka 30 ya Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia (MIMP), unaolenga kujadili masuala mbalimbali ya kisayansi, uhifadhi na biashara yanayohusiana na rasilimali za bahari.

 

Mdahalo huo unaangazia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 30 ya uhifadhi wa bahari, changamoto zilizojitokeza pamoja na nafasi ya jamii katika kuhakikisha rasilimali hizo zinalindwa na kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

 

Aidha, washiriki wanajadili umuhimu wa kutambua na kuhifadhi maeneo yenye umuhimu wa kiikolojia, pamoja na fursa za uwekezaji zinazotokana na rasilimali za bahari na uchumi wa buluu.

 

Majadiliano hayo yanatoa nafasi kwa wadau kubadilishana uzoefu na mitazamo kuhusu namna ya kuimarisha uhifadhi shirikishi, matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na kukuza fursa za kiuchumi zinazowanufaisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi.

slot gacor